SACCOS NI NINI?
NENO SACCOS Ni
Ufupisho wa maneno ya Kiingereza yafuatayo:
Savings
(SA)
Credit
(C)
Co-operative
(Co)
Society
(s)
Maneno
haya ndiyo huunda neno moja SACCOS yaani Savings and Credit Cooperative
Society. Kwa kiswahili
tafsiri rasmi ni chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo.
CHAMA CHA USHIRIKA NI
NINI?
Kwa
mujibu wa tafsiri iliyotolewa na Wizara ya Ushirika na Masoko
Februari 2003 katika sera ya maendeleo ya ushirika.
Chama
cha ushirika ni Muungano wa watu waliojiunga pamoja, kwa hiari
kwa madhumuni ya kufanikisha mahitaji yao kwa kuanzisha na kumiliki chombo chao
kidemokrasia na kuchangia mtaji unaohitajika kwa usawa na
kukubali kuyakabili matatizo na kupata
manufaa kutokana na shughuli zake ambazo
wao hushiriki kikamilifu.
SIFA ZA
KIPEKEE ZA CHAMA CHA USHIRIKA ZIPO SIFA KUU 4 ZINAZOUPA USHIRIKA SIFA
ZA UPEKEE:
1. Ni
Taasisi inayoongozwa na kundi la watu
(Controlled by an association of persons)
2. Ni Taasisi inayoweza miongoni mwa wanachama wake kuwa na watumiaji wa aina moja au zaidi
wa huduma zake (watoaji na wapokea
huduma)
3. Lengo kuu la ushirika siyo kupata faida
kubwa au kuibadili jamii ila kukuza
maslahi ya wanachama wanayoyapata kwa kufanya biashara na chama chao cha
ushirika.
4. Huongozwa na Masharti mtaalum
yanayohakikisha usawa katika kugawana
madaraka (equality in distribution of power) na
uwiano sawa katika kugawana mali ya chama (equity in
distribution of assets). Haya
hutekelezwa kwa kuzingatia misingi 5 ya
ushirika.
v Uwajibikaji
v Demokrasia
v Usawa
v Kuchangia kwa usawa
v Mshikamano
KANUNI MPYA ZA
USHIRIKA
1.Uanachama wa wazi na hiari
2.
Udhibiti
wa kidemokrasia wa wanachama
3.
Ushiriki wa
kiuchumi wa wanachama.
4.
Uhuru
na kujitegemea
5.
Elimu,
mafunzo na habari
6.
Ushirikiano
baina ya wanaushirika
7.
Kujali
jamii
SACCOS nini basi?
Ni :
§ Asasi ya kifedha inayomilikiwa na kuongozwa na
muungano wa watu.
§ Asasi inayomilikiwa kwa pamoja kati ya waweka
Akiba na Wakopaji.
§ Ni asasi
ya kifedha yenye malengo tofauti na yale ya kibenki yanayolenga kukuza
faida za ushirika kwa wanachama wake kupitia akiba zao na mikopo yao,
§ Asasi inayoendeshwa kwa kutumia kanuni maalum
BODI ANZILISHI
INATAKIWA KUFANYA NINI?
Bodi
anzishlishi ya SACCOS huchaguliwa katika Mkutano anzilishi unaongozwa na Afisa
Ushirika (W) au Afisa Ushirika yoytoe aliyeteuliwa na Mrajiri wa vyama vya Ushirika nchini.
Kamati
itakuwa na wajumbe 5 hadi 9. Kamati anzilishi itachagua kutoka miongoni mwao Mwenyekiti na kumteua Katibu
na kutunza kumbu kumbu zake.
KAZI ZA BODI
ANZILISHI
(a)
Kuangalia/Kuamua
aina ya chama wanachama wanachotaka kukianzisha kwa kina na madhumuni/malengo
yake.
(b)
Kutathmini;
Ukubwa wa biashara ya wanachama waanzilishi.
(c)
Kufanya tathmini ya wanachama watarajiwa na kiwango
cha biashara tarajiwa.
(d)
Kufanya
upembuzi yakinifu wa kiuchumi na shughuli za kiutendaji zinazotarajiwa kufanywa
na chama husika kwa kushirikiana na Afisa Ushirika au mtu mwingine yeyote
mwenye ujuzi husika.
(e)
Kuandaa
orodha ya wananchama waanzilishi na kumbukumbu za hisa/mtaji wa chama na
michango kama ilivyopendekezwa katika masharti
ya chama.
(f)
Kuandaa
orodha ya wanachama watarajiwa na kumbukumbu za mtaji au michango yao.
(g)
Kuandaa masharti ya chama chao kwa kushirikiana na
Afisa ushirika.
(h)
Kufanya
jambo lolote muhimu ili
kuwezesha/kufanikisha uandikishaji wa chama tarajiwa.
SOTE
TUNAJUA FAIDA ZA USHIRIKA WA KUWEKA NA
KUKOPA. TUUNGANE TUANZISHE SACCOS YETU.