Tuesday, 28 July 2015

1. SACCOS NI NINI?


SACCOS  NI NINI?


 NENO SACCOS Ni Ufupisho wa maneno ya Kiingereza yafuatayo:

Savings (SA)

Credit (C)

Co-operative (Co)

Society (s)

 Maneno haya ndiyo huunda neno moja  SACCOS  yaani Savings and Credit Cooperative Society.  Kwa  kiswahili  tafsiri rasmi ni chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo.

 CHAMA CHA USHIRIKA NI NINI?

 Kwa mujibu wa  tafsiri  iliyotolewa na Wizara ya Ushirika na Masoko Februari 2003 katika sera ya maendeleo ya ushirika.

Chama cha ushirika ni Muungano wa watu waliojiunga pamoja, kwa hiari kwa madhumuni ya kufanikisha mahitaji yao kwa kuanzisha na kumiliki chombo chao kidemokrasia na kuchangia mtaji unaohitajika kwa usawa na kukubali kuyakabili  matatizo na kupata manufaa kutokana na shughuli zake ambazo  wao hushiriki kikamilifu.

 SIFA  ZA  KIPEKEE ZA CHAMA CHA USHIRIKA ZIPO SIFA KUU 4 ZINAZOUPA USHIRIKA SIFA ZA  UPEKEE:

1.  Ni  Taasisi inayoongozwa na kundi la watu  (Controlled by an association of persons)

2.  Ni Taasisi inayoweza  miongoni mwa wanachama wake  kuwa na watumiaji wa aina moja au zaidi wa  huduma zake (watoaji na wapokea huduma)

3.  Lengo kuu la ushirika siyo kupata faida kubwa  au kuibadili jamii ila kukuza maslahi ya wanachama wanayoyapata kwa kufanya biashara na chama chao cha ushirika.

4.  Huongozwa na Masharti mtaalum yanayohakikisha  usawa katika kugawana madaraka (equality in distribution of power) na  uwiano  sawa  katika kugawana  mali ya chama (equity in distribution of assets).  Haya hutekelezwa kwa kuzingatia misingi  5 ya ushirika.

v  Uwajibikaji

v Demokrasia

v Usawa

v Kuchangia kwa usawa

v Mshikamano

 
KANUNI MPYA ZA USHIRIKA

1.Uanachama  wa wazi na hiari

2.    Udhibiti wa kidemokrasia wa wanachama

3.    Ushiriki wa  kiuchumi wa wanachama.

4.    Uhuru na kujitegemea

5.    Elimu, mafunzo na habari

6.    Ushirikiano baina ya wanaushirika

7.    Kujali jamii

 

SACCOS  nini basi?

Ni :


§  Asasi ya kifedha inayomilikiwa na kuongozwa na muungano wa watu.

§  Asasi inayomilikiwa kwa pamoja kati ya waweka Akiba na Wakopaji.

§  Ni asasi  ya kifedha yenye malengo tofauti na yale ya kibenki yanayolenga kukuza faida za ushirika kwa wanachama wake kupitia akiba zao na mikopo yao,

§  Asasi inayoendeshwa kwa kutumia kanuni maalum

 
BODI ANZILISHI INATAKIWA KUFANYA NINI?

Bodi anzishlishi ya SACCOS huchaguliwa katika Mkutano anzilishi unaongozwa na Afisa Ushirika (W) au Afisa Ushirika yoytoe aliyeteuliwa na  Mrajiri wa vyama vya Ushirika nchini.

 Kamati itakuwa na wajumbe 5 hadi 9. Kamati anzilishi itachagua kutoka  miongoni mwao Mwenyekiti na kumteua Katibu na  kutunza kumbu kumbu zake.

 KAZI ZA BODI ANZILISHI

(a)         Kuangalia/Kuamua aina ya chama wanachama  wanachotaka  kukianzisha kwa kina na madhumuni/malengo yake.

(b)        Kutathmini; Ukubwa wa biashara ya wanachama waanzilishi.

(c)         Kufanya  tathmini ya wanachama watarajiwa na kiwango cha biashara  tarajiwa.

(d)        Kufanya upembuzi yakinifu wa kiuchumi na shughuli za kiutendaji zinazotarajiwa kufanywa na chama husika kwa kushirikiana na Afisa Ushirika au mtu mwingine yeyote mwenye ujuzi husika.

(e)         Kuandaa orodha ya wananchama waanzilishi na kumbukumbu za hisa/mtaji wa chama na michango kama ilivyopendekezwa katika masharti ya chama.

(f)          Kuandaa orodha ya wanachama watarajiwa na kumbukumbu za mtaji au michango yao.

(g)         Kuandaa  masharti ya chama chao kwa kushirikiana na Afisa ushirika.

(h)        Kufanya jambo lolote  muhimu ili kuwezesha/kufanikisha uandikishaji wa chama tarajiwa.

 SOTE TUNAJUA FAIDA ZA USHIRIKA WA  KUWEKA NA KUKOPA. TUUNGANE TUANZISHE SACCOS YETU.

No comments:

Post a Comment